Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza katika taarifa yake ya 19 ya operesheni Nasr 2 kuwa limefanya shambulio la kushtukiza dhidi ya kituo cha uongozi wa operesheni maalumu kinachodaiwa kuwa cha maadui katika eneo la Al-Tanf nchini Syria.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vikosi vya anga vya IRGC vilitekeleza wimbi la 11 la operesheni hiyo kwa kaulimbiu "Ya Aba Abdillah Al-Husayn (as)", likisema shambulio hilo lilifanyika kama jibu la kile ilichokiita mashambulizi ya Marekani dhidi ya wanajeshi wa Iran katika eneo la Bampur, Iranshahr.
IRGC imedai kuwa katika operesheni hiyo ilifanikiwa kuharibu mfumo mmoja wa rada pamoja na helikopta kadhaa zinazotumika katika operesheni maalumu, na kusema kuwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani waliuawa.
Aidha, taarifa hiyo imesisitiza kuwa udhibiti wa Mlango wa Hormuz unaendelea kuwa chini ya uwezo wa vikosi vya majini vya Iran, na kwamba hatua zaidi zitachukuliwa endapo, kwa mujibu wa IRGC, "uchokozi wa Marekani utaendelea."
IRGC Yathibitisha kushambulia kwa kushtukiza kituo cha uongozi wa operesheni za Marekani eneo la Al-Tanf nchini Syria
17 Julai 2026 - 15:18
Msimbo wa Habari: 1841303
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limefanya shambulio la kushtukiza dhidi ya kituo cha uongozi wa operesheni maalumu kinachodaiwa kutumiwa na majeshi ya Marekani katika eneo la Al-Tanf nchini Syria, likisema hatua hiyo ni majibu ya mashambulizi yaliyosababisha vifo vya wanajeshi wa Iran.
Maoni yako